Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Wairan wanaoishi nchini Kenya walikusanyika katika Baraza la Utamaduni la Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran jijini Nairobi kwa ajili ya kuadhimisha kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Bibi Fatima Zahra (a), binti wa Mtume Muhammad (sa).

Hafla hiyo ilijawa na hali ya unyenyekevu, maombolezo na kutambua hadhi tukufu ya Bibi Zahra (a) pamoja na nafasi yake kubwa katika historia ya Uislamu.

Katika shughuli hiyo, Sheikh Raheel Khimji kutoka Taasisi ya Bab Al-Ridha mjini Qom - Iran, alitoa mhadhara mrefu kwa hadhira. Katika mawaidha yake alizungumzia vipengele mbalimbali vya maisha ya nuru ya Bibi Zahra (a), nafasi yake ndani ya Madhehebu ya Ahlul-Bayt (a), mchango wake wa kijamii na kielimu, pamoja na ujumbe muhimu wa shahada yake kwa jamii ya Kiislamu ya leo.

Washiriki wa hafla hiyo pia walisoma sehemu za riwaya kuhusu fadhila na misiba ya Bibi Zahra (a), wakimuenzi bibi huyu mtukufu wa Kiislamu. Shughuli ilihitimishwa kwa dua na maombolezo.

Your Comment